2 870 785 libros electrónicos en 110 idiomas
¿No le conviene? No hay problema. Puede devolverlo en un plazo de 30 días
No se equivocará con un vale de regalo. El destinatario puede elegir cualquier producto de nuestra oferta.
Política de devolución de 30 días
Profesa Kithaka wa Mberia anafundisha na kufanya utafiti katika Idara ya Isimu na Lugha, Chuo Kikuu cha Nairobi, Nairobi, Kenya. Mbali na kufundisha na kufanya utafiti, anajishughulisha na uandishi wa mashairi na tamthilia. Tamthilia yake maarufu iitwayo Kifo Kisimani ilikuwa kitabu cha lazima katika mtihani wa kidato cha nne nchini Kenya kuanzia 2006 hadi 2012. Tamthilia yake nyingine iitwayo Natala ilikuwa kitabu cha kutahiniwa katika vyuo vya walimu, pia nchini Kenya, kuanzia 2005 hadi 2016. Mwandishi amewahi kukariri mashairi yake katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na Kenya, Tanzania, Iran, Marekani, US Virgin Islands, United Arab Emirates, Upolanzi, Ujerumani na Italia.
Mbali na Doa, Kifo Kisimani na Natala, Profesa Kithaka wa Mberia amechapisha vitabu vingine ambavyo ni Mchezo wa Karata (mashairi), Bara Jingine (mashairi), Redio na Mwezi (mashairi), Msimu wa Tisa (mashairi), Rangi ya Anga (mashairi) na Maua Kwenye Jua la Asubuhi (tamthilia). Diwani nyingine zake mbili za mashairi, Mvumo wa Helikopta na Bustani ya Miungu (huenda vichwa hivi vikabadilkika), zinatarajiwa kuchapishwa mwaka
huu na mwaka ujao mtawalia.